| title | Mpangilio |
|---|
React huingiliana na zana kama vile kihariri, TypeScript, viendelezi (extensions) vya kivinjari, na compilers. Sehemu hii itakusaidia kuandaa mazingira yako ya kazi.
Tazama vihariri tunavyopendekeza na ujifunze jinsi ya kuvipanga ili vifanye kazi na React.
TypeScript ni njia maarufu ya kuongeza maelezo ya aina (type definitions) kwenye kodi za JavaScript. Jifunze jinsi ya kuunganisha TypeScript kwenye miradi yako ya React.
Zana za React Developer ni kiendelezi cha kivinjari kinachoweza kukagua vipengele vya React, kuhariri props na state, na kutambua matatizo ya utendakazi. Jifunze jinsi ya kuistakinisha hapa.
React Compiler ni zana inayoboresha kitumizi chako cha React kiotomatiki. Jifunze zaidi.
Nenda kwenye mwongozo wa Anza Haraka ili upate maelezo ya dhana muhimu zaidi za React utakazokutana nazo kila siku.